Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa viwanda na biashara Dk. Seleman Jafo amesema kupitia maonesho ya
48 ya Biashara ya Kimataifa takribani kampuni 150 kutoka China zimeonesha nia
ya kuwekeza nchini.
Ameyasema hayo Julai 13 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya
ufungaji Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,2024 hadi Julai 13, 2024.
“Kampuni nyingi kutoka nje zimekutana na wafanyabiashara wa hapa nchini na
kutoa fursa kwa kutumia masoko ya nje ya nchi kupeleka bidhaa zao. hivyo
Maonesho ya Sabasaba yanaipa fursa Tanzania kushiriki katika maonesho katika
nchi mbalimbali. Amesema Dkt Jafo
Akifafanua zaidi kuhusu kauli mbiu ya maonesho hayo ambayo Tanzania ni
Mahali Salama kwa Biashara na Uwekezaji” Dkt Jafo amebainisha kuwa na kuna
fursa mbalimbali za ufanyaji biashara na uwekeaji Tanzania bara na visiwani,
Aidha Dkt. Jafo amewakumbusha wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa
maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment