Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezitaka Taasisi za Biashara
kuondoa urasimu Ili kukuza biashara nakujenga uchumi wa nchi.
Amesema hayo Julai 13, 2024 wakati akifunga Maonesho ya 48 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama sabasaba yaliyokuwa yakifanyika katika
Viwanja vya Mwl. J. K.Nyerere Jijini Dar es Salaam kuanzia June 28, hasi Julai
13, 2024.
Amesema Serikali zote mbili za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania
zina nia ya kuboresha mazingira ya biashara kwa kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabiri Wafanyabiashara Ili kukuza biashara na uchumi.
Aidha, amebainisha kuwa kupitia maonesho hayo jumla ya masoko tisa(9)
yamepatikana ikiwemo Afrika Kusini, Malawi, Uturuki na Saudi Arabia na kwamba
TANTRADE iendeleze kutafuta masoko zaidi.
Aidha, ameielekeza TANTRADE ifanye uchambuzi wa fursa za masoko mbalimbali
ikiwemo Soko la Eneo Huru la Biashara Afrika (ACFTA), Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo kwa
pamoja kuna nchi 54 zenye idadi ya Jumuiya nane ili wafanyabiashara wayatumie.
Vilevile, amewapongeza wafanyabiashara kwa kutumia fursa ya Maonesho hayo
kukuza mahusiano ya biashara ambayo ni muhimu kwa kuongeza ajira na mapato ya
nchi na kuwataka kuongeza uzalishaji wa bidhaa kama sukari, samaki na miwa Ili
kujitosheleza zaidi na kuweza kuuza nje ya nchi
Aidha amehamasiha sekta binafsi kushiriki katika Maonesho ya Japan Expo
ambayo yatafanyika mwakani April 2025 ambayo yatavutia nchi zaidi ya 180 na
yatakuwa na fursa ya kutangaza bidhaa za Tanzania.
No comments:
Post a Comment