Mfanyabiashara Haidary Gulamali kwa niaba ya wafanya biashara wenzake akichangia jambo wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2024 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo.
................
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHARA wameiomba Serikali iwaruhusu kuingia
nchini na dola za Marekani zenye thamani ya zaidi ya Sh. 10,000 wakati
wakiingia na kutoka nchini kwa ajili ya shughuli zao za kibiashara jambo
litakalosaidia kuinua uchumi wa nchi.
Ombi hilo limetolewa na Mfanyabiashara Haidary
Gulamali kwa niaba ya wafanya biashara wenzake wakati wa kikao kilichofanyika
Julai 12, 2024 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo.
“Mheshimiwa Waziri nchini kwetu hapa unapofika
bandarini au Kiwanja vya ndege hairuhusiwi kuondoka na dola zaidi ya 10,000
kwani kiasi hicho cha fedha ndio kikomo cha kuwa nacho kwa mfanyabiashara au
mtu yeyote atakaye kuwa akisafiri kutoka nchi ya nchi yetu, ”alisema Gulamali.
Gulamali alisema wakati kukiwa na zuio hilo kuna
sheria kwa mtu yeyote atakaye kuwa anaingia nchini na dola zaidi ya 10,000
anazuiliwa.
“Sasa Mheshimiwa Waziri mtu ambaye anatoka Kongo,
Zambia na nchi nyingine mbalimbali analeta nchini dola 10,000 au 20 uchumi wako
si unakuwa na anapowekewa vikwazo hasilete zaidi ya dola hizo inaonesha sheria hiyo
inakuwa inapinga tusikusanye kodi,”
alihoji Gulamali.
Gulamali alisema dola sio dawa ya kulevya ambapo aliomba kuwepo na sheria rafiki ya matumizi yake kama ilivyo nchi nyingine ambazo mfanyabiashara anapokuwa dukani akinunua mahitaji yake anabadilishiwa papohapo.
No comments:
Post a Comment