Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha (Golden Women), wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja huo iliyofanyika jijini Dodoma. Katika hafla hiyo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na afya ya akili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akipokea zawadi kutoka kwa Mhasibu wa Umoja wa Wanawake wa Wizara hiyo, Bi. Lucy Siwiti, mara baada ya uzinduzi wa hafla ya Umoja wa Wanawake wa Wizara hiyo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja huo Bi. Janeth Hiza, Mwenyekiti Bi. Consolata Maimu na Katibu Nyanzala Nkinga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wizara hiyo (Golden women), Bi. Consolata Maimu (wapili kushoto) na Mwenyekiti Msaidizi wa Golden women, Bi. Janeth Hiza, wakiwa katika picha ya pamoja na wastaafu walioagwa katika hafla ya uzinduzi wa umoja huo, jijini Dodoma. Kushoto ni Bi. Shella Juma na kulia ni Bi. Jitihada Lulela na Bi.Mary Mwijage.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi Jenifa Christian Omolo akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha (Golden Women), katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Katika hafla hiyo mada mbalimbali zilkitolewa ikiwemo fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na afya ya akili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akimkabidhi zawadi mwanachama wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha (Golden Women) aliyestaafu utumishi wa umma, Bi. Marry Mwijage, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Wanawake Wizara hiyo wenye kauli mbiu ‘Umoja wa wanawake katika ajira, ni hazina ya maendeleo’, iliyofanyika jijini Dodoma. Katika hafla hiyo mada mbalimbali zilkitolewa ikiwemo fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na afya ya akili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati), akifurahia pamoja na wanachama wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha (Golden Women), wakati wa hafla ya uzinduzi wa umoja huo, iliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa umoja huo, Bi. Consolata Maimu na kulia ni Katibu wa umoja huo, Bi. Nyanzala Nkinga. Katika hafla hiyo mada mbalimbali zilkitolewa ikiwemo fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na afya ya akili.
No comments:
Post a Comment