MKAZI WA DODOMA ASHINDA GARI KAMPENI YA CRDB BENKI NI SIMBANKING - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 31 December 2024

MKAZI WA DODOMA ASHINDA GARI KAMPENI YA CRDB BENKI NI SIMBANKING

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili, akikabidhi namba ya gari ikiwa ni ishara ya kumkabidhi zawadi ya gari mshindi Khamis Majala.

...........................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 Benki ya CRDB imemkabidhi gari jipya Bw.Khamis Majala baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking ambaye amefanya miamala mingi kwenye simu yake ya mkononi katika kampeni iliyolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za SimBanking.


Zawadi hiyo ya gari aina ya Nissan Duals inafanya kufikisha magari mengine manne ambayo yalishatilewa kwa wateja hao na hivyo kufikisha jumla ya magari matano Mpaka sasa ambayo wateja hao wa CRDB wamejishindia.


Akizungumza  Disemba 30,2024 jijini Dodoma kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hiyo Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili,amesema lengo la kutoa zawadi hiyo ni kuhamasisha wananchi kutumia simu za mkononi kufanya miamala.


Ametaja faida za kutumia simu za mkononi kufanya miamala kuwa husaidia kufanya miamala wakati wote, kuokoa muda wa kupanga foleni kupata huduma na kuongeza usalama wa fedha.


"Leo tuko hapa kutoa zawadi kwa mshindi wetu wa gari ambayo imesajiliwa, kujazwa mafuta full tank na bima ya mwaka mzima. Mwanzoni mwa mwaka tulianzisha kampeni ambayo lengo ni kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa kutosha kuhusu huduma za benki zinazopatikana katika simu za mkononi,"amesema Adili.


Ameongeza kuwa :"Wananchi walipokea kampeni hiyo kwa furaha ambayo imesaidia kuongeza miamala kwa asilimia 100 na watu wanaotumia simu za mikononi kwa huduma za kibenki.


Kwa mujibu wa Adili amesema kuwa katika kampeni hiyo walipanga kutoa zawadi ya magari matano ambapo manne wameshayatoa tayari kwa washuindi waliopatikana kupitia kampeni hiyo.


kwa upande wake Meneja wa Biashara Kanda ya Kati Andrew Mheziwa amesema hadi sasa malipo yote yanaweza kufanyika kwa njia ya simu.


"Leo hii tunahitimisha ambapo mshindi wetu atakabidhiwa gari kwa mshindi wetu kutoka Dodoma. niendelee kuwahamasisha wananchi kufungua akaunti za CRDB ambazo zitasaidia kufanya miamala kidigitali,"amesema.


Naye Mshindi wa gari Khamis Majala amesema anaishukuru benki ya CRDB kwa kupata zawadi hiyo huku akihamasisha wananchi kuendelea kufanya miamala kidigitali ili waweze kushinda zawadi mbalimbali.


"Mwanzo nilisikia tu ila sikuamini nilijua ni ya mchongo lakini baada ya kupigiwa simu kuwa nimeshinda ndo nikaamini kumbe ni kweli. Hivyo naomba wananchi waendelee kufanya miamala kupitiaCRDB ili waweze kushinda kama mimi,"amesema MajalaGari alilokabidhiwa Majala.Adili akizungumza katika hafla hiyo.

Meneja wa Biashara Kanda ya Kati Andrew Mheziwa akizungumza wakati wa makabidhiano hayo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages