Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor, kampuni inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan, Ken Aoki (wa pili kushoto) akimkabidhi mmoja wa wateja wa kampuni hiyo, Ucaya Awanga zawadi mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake. Kushoto ni Muhammed Fahmi, ambaye ni afisa mauzo mwandamizi wa Kobe Motor.
Maneja wa kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan ya Kobe Motor, Ananda Shanka akimkabidhi mmoja wa wateja wa kampuni hiyo, Vimal Patel zawadi mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake. Anayeshuhudia kushoto ni Muhammed Fahmi, ambaye ni afisa mauzo mwandamizi wa Kobe Motor.
Muhammed Fahmi (kushoto) Afisa mwandamizi mauzo kutoka kampuni ya Kobe motor Japan inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan akimkabidhi zawadi Mohamedraya Hassam ambaye ni mteja wa kampuni hiyo mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake. Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor, Ken Aoki.
Bendi ya Violist ikitumbuiza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan ya Kobe Motor kwa ajili wateja wake na kufanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor, kampuni inayouza magari yaliyotumika kutoka
Japan Ken Aoki (kulia) akiwa na Muhammed Fahmi (kushoto) ambaye ni afisa
mwandamizi mauzo wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wateja muda mfupi baada ya hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na
kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake. |
KAMPUNI ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan
ya Kobe Motor, imetoa zawadi mbali mbali kwa wateja wake ikiwa ni sehemu ya
kuimarisha uhusiano na wateja pamoja na kusherehekea mafanikio yake.
Ikiwa ni moja kati ya makampuni makubwa ya Kijapan yanayoongoza kwa kuuza
magari kwa ajili ya matumizi binafsi na ya kibiashara sehemu mbali mbali
duniani, Kobe Motor tayari imeshauza magari zaidi ya 150,000 hapa Tanzania.
Akiongea wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa
wateja wake, mkuu wa kitengo cha masoko, Ken Aoki alisema mafanikio ambayo
kampuni hiyo imeyapata ni kutokana na wateja wake waaminifu.
“Leo tunajivunia kampuni yetu kutokana na ukubwa wake pamoja na uwezo wa
kuwafikia maelfu ya wateja hapa Tanzania na sehemu nyingine duniani. Mafanikio
haya tunayojivunia yamepatina kutokana na wateja hawa ambao leo tumejumuika
pamoja kusherehekea mafanikio,” alisema mkuu huyo wa masoko.
Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, iliyoambatana na burudani mbali mbali,
ilichezeshwa droo ambapo wateja wa Kobe Motor walijishindia zawadi mbali mbali
kama simu za mkononi, tablet, komputa mpakato (lap top).
No comments:
Post a Comment