SHIRIKA la nyumba Zanzibar (ZHC) limezindua mradi wa kukopesha nyumba kwa
kushirikiana na Benki ya Azania.
Nyumba hizo zilizojengwa na ZHC zipo visiwanj Pemba na Unguja.
Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo imefanyika leo Februari 14, 2024 kisiwani
Unguja.
Mkurugenzi Mkuu wa ZHC, Mwanaisha Ali Said amesema “Makubaliano haya na
Benki ya Azania yanatoa wepesi zaidi kwa wateja wa shirika letu na kuwaongezea
wigo wa kuwawezesha kununua na kumiliki nyumba bila hofu”.
Naye Meneja Mwandamizi wa Wateja binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay
amesema benki hiyo imejipanga na iko tayari kuwakopesha watakaohitaji nyumba
hizo ambazo gharama zake ni nafuu sana.
“Ninawapongeza ZHC kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na sisi katika
hili. Wameonesha uhalisia wa kuwa shirika linalolenga kumuinua Mzanzibari kwa
vitendo,” alisema
“Sisi Benki ya Azania tuko tayari kuwahudumia kwani hatuna ugeni kwenye
biashara hii, tuna uzoefu wa kutosha na tutawakopesha kwa faida ya chini sana
ya kuanzia asilimia 14 tu ambapo muda wa marejesho ni mpaka kufikia miaka 25”.
Alisema Lohay
No comments:
Post a Comment