BENKI YA NBC NA VODACOM TANZANIA WAUNGANA KUFANIKISHA NBC DODOMA MARATHON 2024 - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 9 July 2024

BENKI YA NBC NA VODACOM TANZANIA WAUNGANA KUFANIKISHA NBC DODOMA MARATHON 2024

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Tumeingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ili kufanikisha maandalizi ya msimu wa tano wa mbio za NBC Dodoma Marathon. Mbio hizi zenye hadhi ya kimataifa zinatarajiwa kufanyika Julai 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Kupitia ushirikiano huo wenye thamani zaidi ya milioni 100, Vodacom Tanzania itakuwa mdhamini Mkuu wa mbio za kilometa 21, hatua ambayo itapeleka mbio hizo za KM 21 sasa kufahamika kama “Vodacom 21Km Dodoma Marathon Race,”. Kupitia makubaliano hayo pia kampuni hiyo itakuwa mshirika wa teknolojia na mawasiliano katika mbio hizi.

Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika mapema leo, Makao Makuu ya Vodacom Tanzania ikihusisha maofisa waaandamizi kutoka pande zote mbili na waandishi wa habari ambapo ikishuhudiwa Mkuu wa Mahusiano ya Umma ya Umma na Mawasiliano wa NBC, Godwin Semunyu na Mkuu wa Mahusiano ya Umma na Vyombo vya Habari wa Vodacom, Annette Kanora wakiwakilisha taasisi zao kwenye makubaliano hayo.

#NBCDodomaMarathon2024 #KataWeseOkoaMaisha


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages