DKT. BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA MODERN INDUSTRIAL PARK - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 24 June 2024

DKT. BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA MODERN INDUSTRIAL PARK

Asisitiza Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akipeana mikono na Mwakilishi wa Kampuni ya Modern Industrial Park, Bw. Yusuf Manzi baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa kampuni hiyo Bungeni jijini Dodoma Juni 24, 2024.
....................................................

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati 

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa Modern Industrial Park wanaomiliki kongani ya viwanda eneo la Kibaha, mkoani Pwani. 

Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 24, 2024 katika ofisi za Naibu Waziri Mkuu Bungeni, jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Biteko amewaeleza wawekezaji hao kuwa Serikali iko tayari kushirikiana nao na kuwapatia umeme kwa ajili ya kuwezesha shughuli za uwekezaji katika eneo hilo.

Naye, Mwakilishi wa kampuni ya Modern Industrial Park, Bw. Yusuf Manzi alisema kuwa eneo hilo lina uwezo wa kubeba viwanda 202 vya aina mbalimbali na tayari miundombinu wezeshi kama maji, Ulinzi na usalama pamoja na barabara vimeshawekwa kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji katika eneo hilo ambalo lina uhitaji wa 200MW za umeme kwa ajili ya kutumika na wawekezaji.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akisalimiana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni hiyo baada ya kufanya nao mazungumzo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni hiyo baada ya kufanya nao mazungumzo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages