BENKI YA ABSA, WADAU MBALIMBALI WAKABIDHI VIFAA TIBA KUIMARISHA UZAZI SALAMA ZANZIBAR - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 24 June 2024

BENKI YA ABSA, WADAU MBALIMBALI WAKABIDHI VIFAA TIBA KUIMARISHA UZAZI SALAMA ZANZIBAR

Makabidhiano ya Vifaa Tiba Kupitia Programme ya “Uzazi ni Maisha Wogging”

 .........................................

Na Mwandishi Wetu

Zanzibar, Tanzania – 24 June, 2023 – SHIRIKA la Amref Health Africa -Tanzania, kwa kushirikiana na Benki ya Absa na Wizara ya Afya ya Zanzibar na Wadau mbalimbali, leo limekabidhi vifaa tiba kupitia program yake ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging’ kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba ili kuimarisha Uzazi Salama Zanzibar. 

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui, amesema jumla ya vituo vya afya 28 vitanufaika moja kwa moja kutokana na programu hii na kupokea vifaa tiba. Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza wakati wa makabidhiano ya Vifaa Tiba.

“Msaada wa utoaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama Zanzibar ni muhimu na inahitajika sana. Jukumu letu kama serikali ni kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa vinapatikana wakati wote na kutumiwa kama ilivyokusudiwa, kwani hiyo ndiyo njia ya kuokoa uhai wa maisha ya Wazanzibari, hasa akina mama na watoto wachanga. Alitoa hakikisho kwamba serikali itahakikisha msaada huo unavifikia vituo vyote vya afya vilivyolengwa Visiwani”,amesema. 

Vile vile, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassoro Mazrui, alipongeza juhudi za Amref na wadau mbalimbali kwa kubuni njia hiyo ya kipekee na kuwaasa wadau zaidi kushiriki ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya uzazi salama hapa Zanzibar. 

Natoa rai kwa kila mmoja wetu kuendelea kushiriki na kuchangia kupitia tovuti yao ya https://wogging.amref.org/ na lipa no. Vodacom 5529421, Tigo 6633523 ili tuendelee kuokoa Maisha ya mama na mtoto. Makabidhiano ya Vifaa Tiba Kupitia Programme ya “Uzazi ni Maisha Wogging.Dkt. Serafina Mkuwa (Meneja program ya Afya ya mama na mtoto) Amref Tanzania, akizungumza wakati wa makabidhiano ya Vifaa Tiba.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, kwa niaba ya Mkurugenzi mkazi wa Amref Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa (Meneja program ya Afya ya mama na mtoto) amesema “Kupitia kampeni hii ya Uzazi ni Maisha Wogging ambayo inafanyika pia kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa afya na makampuni binafsi ambao wanachangia upatikanaji wa vifaa tiba hivi kwa ajili ya uzazi salama. Takribani vituo vya afya 28 vyenye uhitaji mkubwa zaidi ndani ya mikoa mitano ya Zanzibar watanufaika na vifaa hivi. Hii ni awamu ya tatu ya kukabidhi vifaa tiba vilivyopatikana na tutaendelea kukabidhi vifaa vingine kulingana na michango tunavyoipata kutoka kwa wadau waliotuahidi”.

Amref Health Africa Tanzania na Wizara ya Afya Zanzibar zinaendelea kujizatiti katika kuboresha uzazi salama na afya ya uzazi, sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto katika vituo vya afya vya Zanzibar. 

Rabia Aboud, Meneja wa Tawi Benki ya Absa, Zanzibar akizungumza wakati wa makabidhiano ya Vifaa Tiba.

Kwa upande wake ,Rabia Aboud Meneja wa Tawi la Zanzibar Benki ya Absa amesema ushiriki wao ni mwendelezo wa juhudi za benki hiyo katika kutekeleza sera yake ya kurejesha sehemu ya faida yake katika masuala ya kijamii (CSR) ikisukumwa na utayari wa kushirikiana na jamii ili kusaidia sekta ya afya, hasa afya ya akina mama kama moja ya nguzo kuu ya sera hiyo ya Benki ya Absa. 

Rabia Aboud ameongeza kwamba Benki ya Absa inatambua umuhimu wa kuwasaidia wadau wengine kama Amref kwa lengo la kuchangia katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaisha katika maeneo kama afya, na ubora wa kiuchukumi kwa ujumla. 

Programu ya Uzazi ni Maisha Wogging kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo (2022-24) imejiwekea lengo la kukusanya angalau shilingi bilioni moja za kitanzania fedha taslimu, michango na ahadi mbalimbali za kusaidia vifaa tiba. Programu hiyo itaendelea kuwa wazi ikishirikisha kikamilifu na wadau na watu mbalimbali hadi hapo lengo litakapofikiwa. Michango inaweza kutolewa kupitia namba ya Vodacom Lipa 5529421, Tigo 6633523 au kupitia tovuti ya https://wogging.amref.org 

Shirika la Amref Health Africa, tunaahidi kuwa tutaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali kwa kufuata miongozo ya Serikali na Wizara ya Afya ili kuboresha afya ya jamii ya Tanzania.Shukrani maalumu: Tunatoa shukrani pia kwa wadau wetu wote ambao wameshiriki katika kuchangia upatikanaji wa vifaa hivi muhimu ili kuokoa Maisha ya mama na mtoto akiwemo mdau mkuu ABSA Benki, na wadau wengine wakiwemo NBC, NMB Banks, M&D Chemical and surgical LTD, Tanzania Ports Authority , ,ITV/Radio one ,Swahili Sweatshop ,Dalberg Tanzania, CRDB Bank, Siemens Healthcare LLC, Amref Australia, Medical Stores Department (MSD), Rans Company Limited, Cornerstone Solutions Limited, Strategies Insurance ,Madinat Al Bahr, Flying Doctors Africa, Zanzibar Serena Hotel, Titching Pharm Access International, Amref Flying Doctors, Mazrui Building Company, Fortes Garage Ltd, GT Bank, Meraas Perfume Company Limited, Swala Air Cargo, Jeel International Ltd, Amref staff, Amref Health Innovation, Amref International University, Naivera Complex, Laurent & Augustine, Zanzibar Food & Drug, Mambo Leo Digital, LAL Garage, HAI Agency and General, AGOTA, Numpe Industrial Services, Zanzibar Maisha Bora Foundation, Transcend Group of Companies, Notus General Supply, NACOPHA, APECHI, MYSERVICE, Security Printers LTD, Target Lounge, DINARI, AFRIcai, Elpis Company Limited, Super Kitasa JR Motors Limited, Marumaru Hotel, United Nations Office, Nebula Healthcare, Medical Teams International, Deity Company Ltd, na pia wadau wengine wote wakiwemo na watu binafsi. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages