Azimio hilo limepitishwa leo wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa
Benki ya NMB.
Hili ni ongezeko la 26% ukilinganisha na gawio la jumla la Shilingi Bilioni
143.1 tulilolipa mwaka 2022, na kuandika historia mpya ya kuwa gawio kubwa
zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya fedha nchini kwa wanahisa wake.
Mafanikio haya ni matokeo ya mazingira mazuri ya kibiashara yaliyowekwa na
Serikali yetu, imani ya wanahisa na wateja wetu, juhudi za wafanyakazi wetu na
ushirikiano mzuri tulionao na wadau wetu wote.
Tutaendelea kusimamia ahadi yetu ya kudumu katika ukuaji jumuishi na
endelevu kwa ustawi wa jamii tunayoihudumia na uchumi wa nchi yetu ya Tanzania
kwa ujumla.
Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya.
#NMBAGM2024 #NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment