NDEJEMBI AITAKA NMB KUPIMA MATOKEO YA SH BILIONI 2 ZA KAMPUNI CHANGA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 19 October 2026

NDEJEMBI AITAKA NMB KUPIMA MATOKEO YA SH BILIONI 2 ZA KAMPUNI CHANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam, kwaajili ya kufungua Kongamano la Wiki ya Biashara Bunifu (Startup Week 2026), leo tarehe 19 Oktoba 2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi akisikiliza maelezo kutoka Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna kuhusu uwezeshaji katika biashara bunifu, wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wiki ya Biashara Bunifu (Startup Week 2026), linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam, tarehe 19 Oktoba 2026.

Dar es Salaam. Benki ya NMB imetenga Sh bilioni 2 kusaidia kampuni changa za teknolojia, huku ikilenga kuunganisha kampuni 30 na mifumo yake ya kibenki ifikapo mwaka 2030, kutoka sita zilizopo sasa. Benki hiyo pia inatarajia kuanzisha Kituo cha Ubunifu (NMB Innovation Hub) ili kuchochea ukuaji wa biashara bunifu nchini.


Akizungumza katika Tanzania Startup Week 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema kampuni sita tayari zimeanza kuuza suluhisho zao kupitia mifumo ya benki hiyo, huku nyingine tano zikitarajiwa kuunganishwa kabla ya mwisho wa mwaka. Amesema hatua hiyo inazipa kampuni changa fursa ya kufikia wateja zaidi ya milioni 10 wa NMB.


Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameipongeza NMB kwa kuunga mkono ubunifu wa vijana, lakini amesisitiza umuhimu wa kupima matokeo ya uwekezaji huo. Ametaka kuwekwa wazi fedha zilizotumika, idadi ya kampuni zilizonufaika na zilizokua hadi kujiendesha, huku akizitaka taasisi za fedha kusaidia biashara changa zinazokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dhamana za mikopo.


Awali, Meneja wa Ubunifu wa Benki ya NMB, Maria Mwamnyalla, amesema zaidi ya bunifu 300 zimefanyiwa majaribio kupitia NMB Sandbox tangu mwaka 2021. Amesema fedha zilizotengwa zitasaidia kuondoa vikwazo vya kiteknolojia vinavyokwamisha kampuni changa kufikia masoko. NMB imekuwa mdhamini mkuu wa Tanzania Startup Week tangu mwaka 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages