...........................
Na Dotto Mwaibale , Tanga
BENKI ya Uwekezaji Tanzania (TIB), kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, inajivunia mafanikio makubwa ya kuchochea fursa za kiuchumi na kuongeza ajira nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Deogratius Kwiyukwa, akizungumza na na waandishi wa habari katika banda la benki hiyo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika mkoani Tanga, alisema benki hiyo inajivunia mafanikio lukuki yakiwemo ya kutoa fursa za ajira na kuinua uchumi wa nchi.
Kwiyukwa alisema benki hiyo inafanya kazi na sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda, miundombinu, kilimo, ufugaji, Madini, Utalii na uvuvi, kwa lengo la kufikia malengo mapana ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi.
Alisema jitihada kubwa inayofanywa na benki hiyo imeongeza kusukuma mbele maendeleo ya viwanda na kutapunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi hivyo kusaidia taifa kuokoa fedha za kigeni.
Aidha, Kwiyukwa alisema hivi sasa badala ya kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje, fedha hizo zitatumika hapahapa nchini jambo ambalo limesaidia kuchangia ukuaji wa uchumi.



No comments:
Post a Comment