Mkuu wa Idara ya Masoko wa Airtel Ukanda wa Pwani, Mussa Sultan, wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la kampuni hiyo ya simu katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea viwanja vya Usagara, jijini Tanga.
.........................................
a Mashaka Kibaya,Tanga.
MTANDAO wa mawasiliano ya simu za mkononi wa Airtel umeendelea kujiimarisha katika kuboresha mifumo yake ya kifedha, hatua inayowawezesha wadau na wateja wake kupata kwa urahisi huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa na kampuni hiyo.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Aitel Ukanda wa Pwani, Mussa Sultan, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea viwanja vya Usagara, jijini Tanga.
Sultan amesema kuwa ushiriki wa Airtel katika maadhimisho hayo umelenga kutumia fursa hiyo kuuelimisha na kuuhabarisha umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mtandao huo wa simu za mkononi, hususan huduma za kifedha.
Ameeleza kuwa Airtel imejikita zaidi katika kuboresha mfumo wa Airtel Money, ambapo kwa sasa wadau wanaweza kupata huduma nyingi kwa urahisi, ikiwemo wanafunzi kutumia huduma hiyo kulipia ada za shule bila usumbufu.
Aidha, Sultan amesema kuwa kwa sasa hakuna ulazima kwa wafanyabiashara kubeba fedha nyingi wanaposafiri kwenda kununua bidhaa zao, kwani wanaweza kufanya miamala yao kwa usalama kupitia Airtel Money.
Kwa upande mwingine, amesema huduma ya Airtel Money imewasaidia vijana wengi kunufaika kupitia fursa za uwakala, hali iliyowawezesha kujipatia kipato hivyo kumudukujikimu kimaisha.
Akizungumza kuhusu huduma ya uwakala wa Airtel Money, Sultan amesema kuwa mtu yeyote anaweza kujiunga na mfumo huo mradi atimize vigezo na taratibu za kisheria, ikiwemo kuwa na leseni ya biashara pamoja na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN).
Ameongeza kuwa mtandao wa Airtel umeendelea kutoa fursa lukuki za kiuchumi kwa vijana, ambazo zimekuwa zikiwasaidia kujiajiri na kujiinua kiuchumi.



No comments:
Post a Comment