Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Charles Kanuda, akizungumza na waandishi wa habari Januari 22, 2026 katika Maadhimisho ya Wiki ya Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.
.................................
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa elimu ya utambuzi wa noti
bandia kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwakwani mkoani Tanga.
Mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule hiyo, Adrus Mahmoud akizungumza na waandishi wa habari Januari 22, 2026 wakati walipotembea banda la benki hiyo katika
Maadhimisho ya Wiki ya Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Shule ya
Sekondari Usagara jijini Tanga aliishukuru benki hiyo kwa elimu
waliyopewa.
“Tunaishukuru BoT kwa elimu ambayo imetupatia na sisi kwa niaba ya wenzetu ambao
hawakubatika kufika katikakatika maadhimisho haya tutakwenda kuwapa,” alisema
Mahmoud.
Alisema amefarijika amefarijika kupatiwa elimu ya ziada juu
ya kutambua alama za kificho zilizomo kwenye noti ambayo itawasaidia kuzibaini
wakiwa nyumbani kwao na maeneo mengine.
Mwalimu wa shule hiyo, Mwajuma Kileo alisema elimu hiyo
inakwenda kuwasaidia wanafunzi na kuwa mabalozi kwa wenzao ambao hawakuwepo
kwenye ziara hiyo ya mafunzo.
Wakati huohuo Afisa Mwandamizi Mkuu kutoka Kurugenzi ya
Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa benki hiyo, Mwile Kauzeni, mewataka watu
wanaojihusisha na biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila ya kuwa na leseni
kuacha mara moja kwani wanatenda kosa la jinai.
“Tunawaagiza watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume
na utaratibu wafuate sheria ili waweze kufanya kazi hiyo kwa halali kinyume na
hapo wanaikosesha serikali mapato,” alisema Kauzeni.
Kauzeni aliwataka wote wanaofanya biashara hiyo kutembelea
matawi ya benki hiyo ili kujua taratibu za kujisajili au kupitia mtandao wa
benki hiyo.
Kwa upande wake Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa benki hiyo
, Charles Kanuda alisema Serikali imeanzisha mfuko wa udhamini wa mikopo na kwa
mtanzania ambaye atahitaji lakini hana dhamana atapatiwa dhamana mpaka asilimia
75.
Alisema watu wengi wamekuwa wakijaribu kwenda kukopa huku
wakiombwa dhamana yenye thamani kubwa zaidi ya mikopo wanayohitaji hivyo
kushindwa kupata mikopo.
Alisema baadhi ya watu wameshindwa kuchukua mikopo au
kuchukua kiasi kidogo jambo ambalo limeathiri ufanisi wa biashara zao
wanazoziendesha.
Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha ni “Elimu ya fedha , msingi
wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi"
Meneja Msaidizi Sarafu, Joyce Saidimu kutoka Arusha, akiwakabidhi vipeperushi wanafunzi wa shule hiyo.
Afisa Mwandamizi Mkuu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa benki hiyo, Mwile Kauzeni akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo.
Mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule hiyo, Adrus Mahmoud akizungumza na waandishi wa habari
Mwalimu wa shule hiyo, Mwajuma Kileo akizungumzia ziara hiyo ya mafunzo.



No comments:
Post a Comment