...........................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MENEJA wa Bidhaa na Huduma wa Benki ya Biashara (NBC), Richard Bitababaje, amesema ushirikiano wa miaka 7 kati ya NBC na Silent Ocean umeimarisha usafirishaji wa mizigo kwa uhakika na ufanisi.
Akizungumza baada ya semina iliyoandaliwa na Silent Ocean , Bitababaje ameeleza kuwa kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa katika masoko ya kimataifa na inatoa huduma bora za usafirishaji, zikisaidia wateja kufikia bidhaa na masoko kwa urahisi.
Kwa mujibu wake, wafanyabiashara wanapaswa kutarajia fursa zaidi, ikiwa ni pamoja na kupata bidhaa kutoka nchi kama Marekani, Uturuki, India, na Dubai kupitia ushirikiano huo.
No comments:
Post a Comment