.....................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Silent Ocean kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC) wametangaza mikakati ya kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati
kutambua fursa za masoko na bidhaa nje ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Silent Ocean Marekani, Richard Mwandemani, ameeleza mipango
hiyo kupitia semina kwa watumishi wa NBC Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Amesema kampuni hiyo imepanga kuwawezesha wafanyabiashara kuelewa hatua za
kuagiza bidhaa kutoka nje kwa bei nafuu kupitia Silent Ocean.
Aidha, Meneja wa Bidhaa na Huduma wa NBC, Jonathan Bitababaje amesema benki
hiyo ipo tayari kutoa mikopo, ushauri, mafunzo, na kuwaunganisha wateja na
masoko ya kimataifa, ikiwemo Marekani, kwa kushirikiana na Silent Ocean.
No comments:
Post a Comment