Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa zaidi ya shilingi bilioni nne ya sehemu ya faida yake kwa jamii kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, jitihada zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi amesema Benki yake
itaendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo ile inayohusiana na afya.
“Leo, tunapozindua kituo hiki cha afya cha Kizimkazi kilichojengwa kwa
zaidi ya shilingi bilioni 4.4, tunajivunia kuwa miongoni mwa wadau wakubwa
waliofanikisha ujenzi wa kituo hiki muhimu.
Tumechangia kiasi cha shilingi milioni 400 katika ujenzi wa kituo hiki
ambacho kitaleta ahueni kubwa katika upatikanaji wa huduma bora za afya kwa
wakazi wa Kizimkazi na maeneo jirani, " amesema Sabi wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja, Zanzibar
kilichojengwa kwa ushirikiano baina ya benki hiyo na wadau mbalimbali hususani
Taasisi ya Samia Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation.
Katika hafla hiyo, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amesema ushirikiano na
ubia baina ya serikali na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi binafsi ni njia
rahisi zaidi katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa faida ya wananchi.
"Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Taasisi ya Samia
Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya NBC hadi
kufanikisha mradi huu ni muendelezo wa mifano mizuri ya kuigwa…hongereni
sana,’’ amesema Dkt. Kikwete.
No comments:
Post a Comment