SIMBA WA BAHARI NA BENKI YA NBC WAFANYA SEMINA ELEKEZI - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 16 January 2025

SIMBA WA BAHARI NA BENKI YA NBC WAFANYA SEMINA ELEKEZI

Semina elekezi kwa wafanyakazi wa Benki ya NBC jinsi ilivyofanyika.

.............................................

 

Na Dotto Mwaaibale, Dar es Saalam

 

KAMPUNI ya Silent Ocean inayosafirisha mizigo mbalimbali kutoka nje ya nchi kupitia kauli mbiu ya Simba wa Bahari imekutana na wafanyakazi wa Bank ya NBC na kuwapa elimu juu ya faida za kusafirisha mizigo yao  na Simba wa Bahari kutoka Marekani.


Utoaji wa mafunzo hayo uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Richard Mwandemani.


Hatua ya kutoa elimu hiyo ni mwendelezo wa Semina zinazotolewa na kampuni hiyo ambazo zinalenga kuwasaidia Wafanyakazi, Wafanyabiashara,na Wajasiriamali  katika swala la usafirishaji wa bidhaa mbali mbali kutoka nje ya nchi.


Nchi ambazo wanasafirisha ni kutoka China (Yiwu & Keqiao) Dubai, Uturuki, Marekani pamoja na India kuja Tanzania.


Mtu yeyote au mfanyabiashara ambaye anataka kusafirisha mizigo yake kupitia kampuni hiyo yenye uzoefu mkubwa anaweza kuwasiliano nayo kwa kupiga simu namba +255 746 813 813. 

.Mkurugenzi wa Silent Ocean Marekani, Richard Mwandemani akitoa mafunzo kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Washiriki wakifuatilia semina hiyo.
Semina ikiendelea.

Mkurugenzi wa Silent Ocean Marekani, Richard Mwandemani akipokea maswali wakati wa semina hiyo.


Zawadi zikiandaliwa kwa ajili ya washiriki wa semina hiyo.
Mkurugenzi wa Silent Ocean Marekani, Richard Mwandemani (kushoto) akikabidhi zawadi kwa  washiriki wa semina hiyo.


Picha ya pamoja baada ya semina hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages