Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Akiba Dkt. Danford Muyango akizungumza wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa droo ya kwanza ya kampeni 'Twende Kidijitali'
...............................................
Na Mwandishi Wetu
Benki ya Akiba imewashukuru
wateja wake kwa kushiriki katika kampeni 'Twende Kidijitali' na kuwahimiza
kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet
Banking, ACB VISA Card na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa huduma
za kibenki.
Shukrani hizo zimetolewa
jijini Dar es salaam Januari 2025 na Mkuu wa Kitendo cha Biashara wa benki
hiyo, Dkt. Danford Muyango wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa droo ya
kwanza ya kampeni ya hiyo ambapo wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani
wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha zilizowekwa moja kwa moja kwenye
akaunti zao kupitia Benki ya Akiba.
"Kampeni ya 'Twende
Kidijitali' ilizinduliwa mwezi Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya
kibenki kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kushinda
changamoto za kifedha mwezi huu wa Januari kupitia zawadi mbalimbali"
amesema Danford.
Wateja walionyesha furaha na
shukrani kwa Benki ya Akiba kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za
kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na
wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote.
Mmoja wa wateja wa
waliokabidhiwa zawadi na Benki ya Akiba ni Alfayo Zephania ambaye alieleza
jinsi alivyopokea furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo.
"Nilifurahishwa sana na tarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora. Natoa rai kwa wateja wengine kujiunga na Benki ya Akiba ili kunufaika na huduma bora ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakubwa katika biashara zangu” alisema Zephania.
Mteja mwingine, Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni hiyo ya 'Twende Kidigitali'.
Pia Benki ya Akiba
imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na kuwasihi
waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki hiyo ili kunufaika zaidi. Meneja Mwandamizi Benki ya
Akiba, Magreth Mwasumbi (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki
hiyo walioibuka washindi wa kampeni ya 'Twende Kidigitali'.
No comments:
Post a Comment