RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA BENKI YA NMB - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 January 2025

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA BENKI YA NMB

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, akiambatana na viongozi wengine wa Benki ya NMB, amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kutoa Salaam za Mwaka Mpya 2025, kutoa taarifa ya maendeleo na mafanikio ya Benki ya NMB kwa mwaka 2024 na mwisho, kuonyesha mwelekeo wa Benki yetu na Mkakati wake wa Mwaka 2025 unaolenga kutoa huduma bora kwa wateja wetu pamoja na kuboresha huduma za kibenki zinazotolewa kwa Watanzania nchini kote.

Mwaka 2024, Benki ya NMB imepata mafanikio makubwa katika sekta ya kifedha, ikiwa ni pamoja na kuwa Benki ya kwanza Afrika Mashariki kuorodhesha Hati fungani ya Uendelevu kwenye soko la Hisa la London na utoaji wa huduma bora za kifedha kwa wananchi. Benki imetambuliwa na Jarida la Euromoney kama Benki bora zaidi Tanzania kwa mara ya 11 kwenye miaka 12.

Kupitia malengo ya mwaka huu 2025, benki yetu imeahidi kuendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali katika kujenga uchumi wa nchi yetu huku tukiendelea kutoa huduma bora zaidi kupitia mtandao wetu wa kibenki uliosambaa nchi nzima na kuwafikia wananchi wote.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages