Wanafunzi wa Shule za Dar es Salaam wakipata Elimu ya Fedha kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
.....................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa elimu ya fedha na umuhimu wa
uwekaji akiba kwa wanafunzi wa Dar es Salaam kupitia mradi wa Natokaje Digital.
Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa fursa kwa wanafunzi hao kujifunza masuala ya
kifedha ili kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba, kubuni mawazo ya biashara
sambamba na kutambua namna ya kutumia taasisi za kifedha ikiwemo benki ya NBC
ili kujinufaisha kiuchumi.
Semina fupi kuhusu mafunzo hayo ilifanyika katika Tawi la Corporate lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao wa shule za Dar es Salaam wakipatiwa elimu hiyo ya fedha.
Elimu ya fedha ikitolewa kwa wanafunzi hao.
Wanafunzi hao wakiondoka kwenye benki hiyo baada ya kupatiwa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment