Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) inawahimiza wananchi wote kwa ujumla
kwenda kufungua akaunti ya malengo ambayo ni muhimu sana.
Akaunti hiyo ya malengo inakupa mtu husika
nafasi ya kuweka akiba kidogo kidogo na kupata riba hadi ya 7%.
" Yapi malengo yako uliyopanga kutimiza ndani ya mwaka huu mpya wa
2025," benki hiyo inakuuliza wewe ambaye bado hujafungua akaunti hiyo.
Benki ya NBC inakuhimiza tena na tena kufungua akaunti hiyo ili ufanikishe
malengo yako yote na inatumia fursa hiyo kuwakaribisha kwenye matawi yao yote
kote nchini kwa ajili ya kwenda kufungua akaunti hiyo ya malengo.
No comments:
Post a Comment