Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Benki ya CRDB imezindua huduma ya mkopo maalum kwa ajili ya ada ya shule wa kiasi cha hadi shilingi milioni kumi na mbili (12,000,000) inayofahamika kama ADA LOAN.
Uzinduzi wa huduma hiyo inayopatikana kirahisi kupitia App pendwa
nchini ya SimBanking uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu wa
Fedha, Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo pamoja na wageni waalikwa na
wadau mbalimbali waliohudhuria wakiwemo wazazi, walimu, Wakurugenzi wa tasisi
za elimu na wanafunzi wa shule.
Benki ya CRDB inaendeleza jadi ya kutoa huduma za kibunifu na rahisi zaidi
nchini.
No comments:
Post a Comment