Na Mwandishi Wetu, Mara
Benki ya CRDB imezindua tawi jipya linalofahamika kama Tawi la CRDB Mugango, katika Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara.
Uzinduzi wa tawi hilo ulipambwa na uwepo wa mgeni rasmi, Gerlad Musabila Kusaya, Katibu Tawala Mkoa Mara, akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa. Sospeter Muhongo.
Pia, Benki ya CRDB iliongozwa na Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa ambaye naye pia aliambatana na baadhi ya viongozi wa Benki akiwemo Meneja wa Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta, Meneja wa tawi la Mungango, Abdalla Magoe pamoja na Meneja wa tawi la Musoma, Jarome Mwenda.
Uzinduzi wa tawi hilo unakwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma za
kibenki na kuchochea shughuli za maendeleo mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment