Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya CRDB, Ndugu Abdulmajid Nsekela akipokea tuzo
ya shukrani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt.
Doto Biteko pamoja na mgeni rasmi Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Tuzo hii
imetolewa kwa kutambua mchango wa Benki ya CRDB kama mdhamini wa tukio kubwa la
siku ya walimu duniani, lililong’ara huko Bukombe.
Tunatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu kwa kutambua mchango wa Benki ya CRDB, na kwa hakika tutaendelea kuwa pamoja katika kuthamini jitihada za walimu nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya CRDB, Ndugu Abdulmajid Nsekela
No comments:
Post a Comment