BENKI YA NMB MTWARA YAHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 12 October 2024

BENKI YA NMB MTWARA YAHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Wananchi wakishiriki Jogging kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa uandikishwaji kwenye daftari la kudumu la mpiga kura. Jogging hiyo iliandaliwa na Benki ya NMB Mkoa wa Mtwara

..............................

Na Musa Mtepa, Mtwara

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara DC, Abeid Abeid Kafunda, ameshiriki katika Jogging ya kuhamasisha wananchi, iliyofanyika leo tarehe 12 Oktoba 2024, kwa ushirikiano wa Benki ya NMB.

Zoezi ambalo limeandaliwa ili kuhamasisha wananchi kushiriki katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura, ambalo lilianza tarehe 11 Oktoba 2024.

Katika hotuba yake mbele ya wananchi wa Mkunwa, Kafunda amesisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, akiwataka wananchi  kushiriki kikamilifu.

Kwa upande mwingine, Dismas Prosper, Meneja wa Kanda wa NMB, ameelezea kuwa benki hiyo inatumia fursa ya NMB Kijiji Day kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zao za benki.

Prosper ameongeza kuwa ni muhimu wananchi wawe na uelewa mzuri wa huduma zinazotolewa na benki hiyo ili kuweza kuzitumia vyema.

Wananchi wakishiriki Jogging iliyofanyika katika kijiji cha Mkunwa Halmashauri ya Mtwara vijijini (Picha na Musa Mtepa) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages