Meneja Maendeleo na Biashara wa Benki ya NBC Tawi la Singida, Olairivan Elineema, akizungumza kwenye mahafali ya 16 ya wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dr. Ali Mohammed Shein yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
.................................
Imeandaliwa
na Dotto Mwaibale, (0754-362990)
WANANCHI wa
Kata ya Misughaa iliyopo Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida, wametakiwa kuweka
akiba za fedha zao kwenye Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ili ziweze kuwasaidia kwa mambo mbalimbali
pamoja na kuwasomesha watoto wao.
Ombi hilo
limetolewa na Diwani wa Kata hiyo, Selemani Musa wakati akizungumza kwenye
mahafali ya 16 ya wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dr.
Ali Mohammed Shein yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Awali
akizungumza kwenye mahafali hayo diwani huyo aliwaomba wazazi na walezi kujenga
tabia ya kutoa chakula kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi wa shule hiyo wanapokuwa
shuleni.
“Tujitahidi
kuwa changia watoto wetu liche wakiwa shuleni ili waweze kusoma kwa mfululizo
na bila ya kukosa chakula,” alisema Musa.
Alisema kuwatunza wanafunzi hao na kuwapa
chakula kutawawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao ambapo aliomba
utaratibu huo wa chakula uanzie shule za msingi.
Akizungumzia
kuhusu utunzaji wa akiba za fedha zao alisema wananchi wengi wa kata hiyo ni
wakulima hivyo wakishavuna na kuuza mazao yao aliwaomba fedha zao wakatunze kwenye Benki ya
Taifa ya Biashara ambapo zitakuwa salama.
“Niwaombeni
mkatunze fedha zenu benki kwani zitawasaidia kwa ajili ya kuwasomesha watoto
wenu na kupata mahitaji yenu mengine,” alisema Musa.
Meneja Maendeleo na Biashara wa Benki ya NBC Tawi la Singida, Olairivan Elineema ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo akizungumza kwa niaba ya Meneja wa benki hiyo tawi la Singida, alipongeza kazi nzuri inayofanywa na walimu kwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi na akapongeza uratatibu wa utoaji wa lishe kwa wanafunzi ambapo benki hiyo itaendelea kutoa chakula kwa ajili ya watoto hao.
Aidha,
Meneja huyo ametoa wito kwa wananchi watakaohitaji kupata elimu ya fedha
wawasiliane na benki hiyo kwani muda wote wapo tayari kutoa elimu hiyo pasipo malipo yoyote.
Katika hatua nyingine Meneja huyo ameahidi kuwafungulia akaunti na kuwawekea Sh. 50,000 wanafunzi wa kwanza watatu watakaoongoza kufanya vizuri kwenye mtihani wao na kupata alama za juu.
Diwani wa Kata ya Misughaa, Selemani Musa akizungumza kwenye mahafali hayo.
Diwani wa Kata ya Misughaa, Selemani, akiteta jambo na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dr. Ali Mohammed Shein, Jackson Maruma.
Wahitimu wakitoa burudani
Skauti wakitoa heshima wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma , akizungumza kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment