KATIBU MTENDAJI NEEC: MIKOPO YA ALISIMIA 10 NI MUHIMU KWA WANANCHI - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 3 October 2024

KATIBU MTENDAJI NEEC: MIKOPO YA ALISIMIA 10 NI MUHIMU KWA WANANCHI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Taifa (NEEC) Bi. Beng’i Issa, akizungumza na Wajasiriamali wa Mkoa wa Singida wakati wa hafla ya kuwakabidhi  Programu ya Imarisha Uchumi na Samia (IMASA) ambayo inasimamiwa na Baraza hilo. Hafla hiyo imefanyika Oktoba 3, 2024.

................................

Na Mwandishi Wetu, Singida

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Taifa (NEEC) Bi. Beng’i Issa, amesema mpango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri za Wilaya kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu ni wa muhimu kwani inawasaidia wananchi.

Issa ameyasema hayo kwenye mkutano wa NEEC na viongozi wa Mkoa wa Singida ambapo Mkuu wa mkoa huo Halima Dendego alikuwa Mwenyekiti.

“Mikopo ya asilimia 10 ambayo imeanza tena kutolewa na Halmashauri zetu kwa makundi hayo  ambayo ilikuwa imesitishwa kwa muda ni ya muhimu na imekuwa ikisaidia sana  kwani imejielekeza zaidi kwa Wananchi kiuchumi” alisema  Issa.

Alisema katika nchi nyingi za Afrika ni Tanzania pekee ambayo imeweka utaratibu wa kutoa mikopo ya aina hiyo hivyo tuna kila sababu ya kujivunia kutokana na utaratibu huo mzuri uliowekwa na Serikali.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia imedhamiria kuwawezesha Wananachi kiuchumi katika Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na ili kufanikisha jambo hilo Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali zitashiriki kuhakikisha Wananchi wanawezeshwa.

Alisema Serikali za Mikoa zitakuwa na jukumu la kuhakikisha program hiyo ambayo itajulikana kama “ Imarisha Uchumi na Samia (IMASA)  inatekelezwa.

Alisema program hiyo inasimamiwa na Ofisi ya Rais Ikulu, kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, na itafanyika katika mikoa na wilaya za Tanzania bara na Visiwani.

Issa alisema baraza hilo kupitia programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia imekuja kuwakwamua wanawake, vijana na makundi maalumu kufanya shughuli za kijasiriamali.

Alisema hatua ya kwanza ya proramu hiyo itahusisha uandaaji wa kanzi data ya walengwa,utambuzi wa shughuli za kiuchumi za wadau na mahitaji maalumu ya uwezeshaji, kwa vikundi vilivyotambuliwa au sajiliwa vya wanawake,vijana na watu wenye mahitaji maalumu.

Alisema awamu ya pili itahusisha uandaaji wa proramu maalumu za uwezeshaji kiuchumi kwa makundi yaliyorasimishwa, kulingana na mahitaji yaliyoonekana katika uchakataji wa takwimu.

“ Ili programu hii iweze kuleta tija na kuwa endelevu, ipo haja ya wadau mbalimbali kuweza kushirikishwa hivyo wito wangu ni kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali ya Mkoa, Wilaya na wadau wote wa maendeleo katika utekelezaji wa programu za uwezeshaji kwa makundi husika,” alisema Issa.

Aidha, Issa alisema kuwa Baraza la Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi litaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa programu kwa kushirikisha wadau wa maendeleo, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wote katika Majiji na Manispaa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego akizungumza kwenye mkutano huo alisema mkoa huo una kwenda kupindua meza kutoka kwenye uteja wa kuitwa Singida ni masikini na kuwa wao sio masikini.

“Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akisema ili upambane na umasikini lazima uwe na vitu kadhaa cha kwanza ikiwa ni ardhi ambayo kwa Singida ipo ya kutosha ina rutuba nyingi na maji ya kutosha na cha pili likiwa ni watu ambao wapo na ni makini hivyo habari ya kuitwa masikini hiyo haipo kwani tumeanza kuchangamkia fursa mbalimbali,” alisema Dendego huku akishangiliwa.

Dendego aliwataka Wananchi wa Mkoa wa Singida kuendelea kukuza uchumi wa mkoa huo kuanzia ngazi ya kaya na kuwa safari hiyo ya kuutafuta uchumi wamekwisha ianza hawatarudi nyuma na atahakikisha kila nyumba inafikiwa kwa kuipatia elimu na kuwezeshwa kwa kupatiwa fedha, maarifa na ardhi kupitia program mbalimbali.

Aidha aliwata vijana kuacha kucheza 'pool' badala yake wafanye kazi na akatoa wito kwa wazazi kuacha tabia ya kuwalea watoto hao bila ya kuwapa shughuli za kufanya na kuwa program hiyo imefika kwa wakati na wana Singida wapo zaidi ya tayari.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akitoa taarifa fupi ya mkoa kwenye mkutano huo alisema pato la Mkoa wa Singida limeongeza kutoka Sh. Trilioni 3.2 kwa mwaka 2022 hadi kufikia Sh. Trilioni 3.39 kwa mwaka 2023 huku pato la kila mtu likifikia Sh. Milioni 1.6  kwa mwaka 2023.

Alisema mwaka jana licha ya Serikali kusimamisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 lakini Mkoa wa Singida uliendelea kusajili vikundi mbalimbali ambapo walisajili vikundi 1,432  vikundi vya wanawake vikiwa vingi na vijana vikiwa 344 na 82 vya watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akizungumza na Wajasiriamali hao.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, akizungumza kwenye mkutano huo. 
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Neema Mwakatobe, akizungumza.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Singida, Emmanuel Kishosha, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Taifa (NEEC) Bi. Beng’i Issa, akiserebuka na Wajasiriamali wa Mkoa wa Singida wakati wa mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajasiriamali wakijaza fomu kwa ajili ya kujiunga na programu hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bertha Nakomolwa ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Singida, Martha Kayaga,Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Taifa (NEEC) Bi. Beng’i Issa, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego  na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali.Wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano huo.

Mkutano huo ukiendelea.
Wanawake na Samia Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages