...........................
Na Mwandishi Wetu, Lindi
Wawekezaji wa ndani Mkoani Lindi wametakiwa kujisajili na kusajili miradi
yao kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kutambuliwa na kunufaika na
faida mbalimbali kama vivutio vya kikodi na kupata misamaha ya ushuru wa
forodha na kodi ya ongezeko la thamani.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati
akifungua semina kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa wawekezaji,
wafanyabiashara na wajasiriamali Mkoani humo iliyoandaliwa na kituo cha
uwekezaji Tanzania (TIC).
Semina hiyo ni sehemu ya kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa
ndani inayoendelea nchini.
Ndemanga ameesema wawekezaji pindi wanapojisajili na kutambulika inasaidia
Serikali kuwafahamu wawekezaji nchini na kuwasaidia katika utekelezaji wa
miradi yao pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.
Akizungumzia faida za wawekezaji kujisajili TIC Meneja wa uhamasishaji
kutoka katika kituo hicho Felix John amesema ni pamoja na kuvutia mitaji,
kuleta tecknologia mpya hapa nchini,kutengeneza ajira kwa vijana wanaohitimu
kutoka kwenye shule na vyuo mbali mbali nchini.
Aidha, Felix ameeleza kwa kipindi cha kuanzia januari hadi julai 2024 jumla
ya miradi 500 imesajiliwa na ITC na matumaini yao ni kwamba miradi hiyo
ikitekelezwa kwa ufanisi itaenda kuzalisha ajira takribani 121,000.
No comments:
Post a Comment