Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw.
George Mbesigwe, akizungumza wakati wa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na
Wizara ya Fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo kujiwekea akiba,
mikopo, uwekezaji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani humo.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Glory Uisso, akizungumza na baadhi ya
wakazi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, baada ya kumalizika kwa semina ya
elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha ambapo mada mbalimbali zilifundishwa
ikiwemo kujiwekea akiba, mikopo, uwekezaji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo
mkoani humo.
Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha,
Wizara ya Fedha Bw. Salim Khalfan Kimaro, akiitambulisha Timu ya Wataalamu
kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Lindi kutoa elimu ya fedha, kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. George Mbesigwe (katikati)
na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ruangwa Bw. Rashid Namkulala.







No comments:
Post a Comment