BADRU AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA BIASHARA NCHINI - UMOJA BANKING BLOG

Home Top Ad

MABENK

Post Top Ad

Tuesday, 13 August 2024

demo-image

BADRU AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA BIASHARA NCHINI

Untitled-2

* Wawekezaji Faida Fund juu takriban 60%! 

* Faida, Thamani, Ukubwa wa Mfuko Vyapaa! 

* Faida Kuongezeka, Mifumo Kuboreshwa! 

(Aishukuru Serikali, Wadau kwa Mafanikio.


RAZAK
Mkurugenzi Mkuu PSSSF, Abdul-Razak Badru

............................... 

Na Derek Murusuri, Royal Publishers, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wawekezaji wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), Bw. Abdul-Razak Badru, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha mazingira ya biashara nchini, hadi Bodi yake kupata Mafanikio makubwa.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kusimamia na kuweka mazingira bora ya biashara nchini,” alisema.

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, Badru, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), alibainisha kuwa Faida Fund imepata ongezeko kubwa la idadi ya wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa thamani ya Mfuko, kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya biashara nchini.

“Kwa kipindi kilichoishia Juni, 2024, idadi ya wawekezaji ilikua na kufikia 4,806 sawa na ongezeko la asilimia 58 la Wawekezaji waliojiunga katika Mfuko, ukilinganisha na kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni, 2023 ambapo idadi ya wawekezaji ilifikia 2,041,” alisema Bw. Badru.

Mwenyekiti huyo alikuwa akiwasilisha taarifa yake ya mwaka ulioishia Juni, 2024, kwenye Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wawekezaji wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

“Kwa kipindi kilichoishia Juni, 2024, idadi ya wawekezaji ilikua na kufikia 4,806 sawa na ongezeko la asilimia 58 la Wawekezaji waliojiunga katika Mfuko, ukilinganisha na kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni, 2023 ambapo idadi ya wawekezaji ilifikia 2,041.” 

Faida kwa Wawekezaji ilikuwa kubwa ikilinganishwa na kigezo linganifu (performance Benckmark). Kwa kipindi cha miezi nane (8) ya mwanzo kilichoishia 20 Juni, 2023, faida iliyopatikana ilikuwa asilimia 10.0 na imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 12 kwa kipindi kilichoishia 30 Juni, 2024.

Mafanikio mengine makubwa ya kujivunia kwa uongozi mahiri wa mfuko, ni kuongezeka kwa thamani halisi ya mfuko, kutoka 15.6bil./- Juni 2023 hadi 25.6 bil./- kufikia Juni, 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *