..................................
Na Mwandishi Wetu,
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB)
imesema inajivunia kuwa sehemu ya mradi wa reli ya kisasa (SGR) uliozinduliwa
hivi karibuni kwa safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Akihutubia katika uzinduzi huo jijini Dodoma, Mheshimiwa Rais Dk. Samia
Suluhu Hassan aliuelezea mradi huo kuwa kielelezo cha maendeleo makubwa ya
kimiundombinu na ya taifa kwa ujumla na kwamba Kuanza kwa mradi wa SGR ni hatua
muhimu katika kutimiza ndoto ya kuwa na miundombinu ya usafiri wa haraka,
rahisi na wa kuaminika.
Alifafanua kwamba matokeo ya mradi yanaweza yasionekane mapema, lakini
lengo la mradi ni kutoa huduma kwa taifa na mchango wake katika kuwezesha
biashara za kimataifa na maendeleo ya nchi na kuwa Sehemu ya mradi huu
inayoendelea kujengwa kuelekea Kigoma mpakani mwa nchi za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo inaonyesha namna mradi huu utakavyonufaisha uchumi wa
nchi hasa sekta ya utalii.
Benki ya TCB imepewa heshima kuwa benki mdau namba moja katika mradi huu wa
kimageuzi kwa kuwezesha mchakato wa kuagiza vichwa vya treni na mabehewa ya SGR
na kutoa mikopo kwa wakandarasi wa Yapi Merkezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayo amesema Lengo lao ni
kuhakikisha kwamba wateja wanafikiwa na kunufaika na huduma za mradi wa SGR
kupitia mawakala walioenea nchi nzima na uwezo mkubwa wa programu ya TCB
Popote, wanamwezesha kila mmoja kujionea urahisi na uhakika wa usafiri wa
kisasa.
Aidha Mihayo ameeleza kuwa Sambamba na hilo , benki ilishinda zabuni ya
kutoa huduma za ukusanyaji wa nauli kwa njia za kidijiti ikiwemo kupitia
mashine za kukatia tiketi (Ticket Vending Machine) hali kadhalika, programu ya
simu ya TCB Popote inayomwezesha mteja kujifungulia akaunti kwa kiasi cha
shilingi 1,000 tu, inarahisisha ukataji wa tiketi za SGR mahala popote nchini.
Wateja pia, wanaweza kununua tiketi zao bila usumbufu kwa mawakala 7000 wa
Benki ya TCB waliopo nchi nzima, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa tiketi na
, hivi sasa kadi za ATM zinaweza kutumika katika mifumo ya PoS na mashine za
kukatia tiketi (TVM) zilizopo katika stesheni zote.
Mihayo amesema Katika kuwezesha mfumo kufanya kazi kwa ufanisi, Benki ya
TCB imezindua mfumo wa malipo wa QR code kwa abiria ili kuwawezesha kutumia
mfumo wa PoS bila kuhitaji intaneti kuzuia makosa ya kimfumo.
Aidha, ubunifu wa mfumo wa kimawasiliano unaotumia akili mnemba kupitia
mtandao wa WhatsApp unawezesha upatikanaji wa huduma za SGR kwa urahisi na
kwamba , makusanyo ya manunuzi ya tiketi yameunganishwa na mfumo wa GePG ili
kuendelea kujenga pato la nchi.
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ni taasisi ya kifedha inayoongoza katika
utoaji wa usuluhisho wa kifedha unaolenga kukidhi mahitaji wa wateja wake na
imekijipambanua katika uchumi jumuishi na maendeleo ya kiteknolojia, Benki ya
TCB inajizatiti kuboresha huduma za kibenki na kuchangia katika ukuaji wa
uchumi nchini.
No comments:
Post a Comment