I&M BANK WAJA NA HUDUMA YA KIBENKI KUPITIA WHATSAPP - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 8 August 2024

I&M BANK WAJA NA HUDUMA YA KIBENKI KUPITIA WHATSAPP

I

Na Mwandishi Wetu

 

BENKI  ya I&M ikiwa katika kusherehekea kutimiza miaka 50 ya utendaji kazi na ufanisi, imeanzisha huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Banking iliyoboreshwa ili kuwarahisishia huduma wateja wao, huduma hiyo ambayo inapatikana kupitia WhatsApp itakuwa inarahisisha utoaji wa huduma mbalimbali za kibenki ikiwa ni pamoja na kuangalia salio la akaunti papo kwa papo, kupokea taarifa za miamala pamoja na kuhamisha au kutuma fedha kirahisi.

Hayo na yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Zahid Mustafa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika uzinduzi huduma hiyo, huku akibainisha kuwa, benki hiyo inaendelea kufanya ubunifu kwa mustakabali endelevu na kuunga mkono mabadiliko ya kidijitali nchini.

“Sisi kama I&M sio tu kwamba hii ni bidhaa yetu ya kwanza bali tupo tunajikita zaidi kwenye dhamira kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali lakini pia tumeingia ushirikiano na Airtel inaitwa kamilisha ambapo tunaweza kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwapa huduma bora zaidi,” amesema Mustafa.

Mtendaji mkuu huyo, amesema dhamira yao ni kuhakikisha wanaondoa matumizi ya karatasi kwenye utoaji huduma kwa wateja wake na badala yake kila kitu kitakuwa kinafanyika kwa njia ya kidigitali ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono ama kuchangia Dira ya serikali ya Tanzania ya uchumi wa kidijitali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Naye Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja katika benki hiyo Simon Gachachi amesema kuwa wamekusudia kuwekeza katika kujenga utendaji zaidi na vipengele vinavyofanya kazi kwa washirika wao wa teknolojia, ambapo pia katika kuboresha zaidi huduma hiyo, amesema mwezi Septemba watazindua namna mteja ataweza kulipa kodi na malipo mengine ya serikali kupitia WhatsApp kwa kutumia mifumo mbalimbali.

Kwa upande wake Meneja wa bidhaa za kidijitali wa benki hiyo Adam Emmanuel ameeleza kuwa huduma hiyo walianzisha tangu mwaka 2021 ambapo wamefanya maboreso mbalimbali ikiwemo kuwaruhusu wateja wapya kujisajili na kufungua akaunti zao wenyewe.

Aidha huduma nyingine ni pamoja na uwezo wa kujisajili mwenyewe unaotumia teknolojia ya AI, muonekano ulioboreshwa kwa mtumiaji, msaada kwa wateja kwa kutumia AI na sehemu ya maswali na majibu yanayoulizwa mara kwa mara.

“Mchakato wa usajili ni rahisi tu ambapo ni sevu namba ya WhatsApp Banking iliyothibitishwa ya I&M Banki +255 755 674696 kisha tuma neno habari halafu fuata maelekezo”, amesema AdamU.

Maeneo ama vipengele muhimu ambavyo vitakuwepo kwenye maboresho hayo kwaajili ya kurahisisha huduma kwa wateja ni pamoja na, huduma ya Kufungua Akaunti, ambapo Mteja anaweza kufungua akaunti yeye mwenyewe ndani ya siku moja, usimamizi wa akaunti ikiwemo kuangalia salio na kupata taarifa za akaunti yake bure, uhifadhi wa mnufaika, hifadhi kwa urahisi namba ya mnufaika kwaajili ya kufanya miamala.

 

Vipengele vingine ni pamoja na kuhamisha Fedha, ambapo mteja anaweza kuhamisha fedha kwenda akaunti ndani ya benki, kutuma fedha kwenda mitandao ya simu, kama vile; M-Pesa, Tigo Pesa, Halopesa na Airtel Money, malipo ya bili mbalimbali, ikiwemo LUKU, DAWASCO, Ving’amuzi nk, kununua muda wa maongezi, kuchatina mtoa huduma moja kwa moja. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages