Rais Mwinyi ametembelea banda hilo alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya
saba ya Kilimo (nane nane) Zanzibar tarehe 3/8/2024.
Katika banda la TADB Mhe. Dkt. Mwinyi amepokelewa na Kaimu Meneja wa Kanda
ya Zanzibar, Bw. Michael Madundo na kupatiwa muhtasari wa maendeleo ya benki
ikiwemo taarifa ya utolewaji wa mikopo, idadi ya wanufaika wa mikopo ya benki
Zanzibar pamoja na:
✅️ Jitihada zinazofanywa na
benki katika kutoa elimu ya fedha na kilimo biashara Zanzibar
✅️ Mendeleo ya Mradi
Shirikishi wa Wasindikaji, Wazalishaji wa Maziwa Tanzania (TI3P) ndani ya
Zanzibar
✅️ Maendeleo ya Mfuko wa
Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS)
🟢 Mhe. Dkt. Mwinyi pia
alipata nafasi ya kuona kazi za wanufaika wa TADB ikiwemo Kampuni ya Bin Mwewe
wakulima wa Matunda na mbogamboga, Shemsa Taraba na Kampuni ya MPF wafugaji wa
kuku wa mayai.
No comments:
Post a Comment