Mkurugenzi ZIPA , Saleh Saad Mohamed
.............................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MAMLAKA ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imekutana na Ujumbe kutoka Chuo
cha Biashara CBE kwa majadiliano na maandalizi ya ujenzi wa Chuo hicho hapa
Zanzibar katika maeneo huru ya Uwekezaji Fumba.
Akizungumza na Ujumbe huo Ofisini kwake ZIPA Maruhubi Mkurugenzi ZIPA , Saleh Saad Mohamed amesema Uwekezaji huo hapa Zanzibar utaondoa usumbufu kwa
Wazanzibar watakaotaka kujifunza, sambamba na kuwapunguzia gharama za masomo.
Mkurugenzi Saleh amesema CBE na ZIPA wanaweza kufanya kazi kwa pamoja
kutokana na ufanano wa mahitaji yao kiutendaji na kitaaluma kutokana CBE ni
Chuo cha Biashara na ZIPA inatoa huduma za Uwekezaji na Taaluma yake.
Amesema ZIPA ili iendane na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia yanayoikumba
dunia ni lazima watumishi wake wapatiwe mafunzo ya mara kwa mara ili
kukabiliana na mabadiliko hayo.
Nae Mkuu wa Chuo Prof. Tandi Lwoga amesema CBE itayafanyia kazi yale yote
yaliyopendekezwa na Mkurugenzi ikiwemo suala zima la mafunzo kwa watumishi wa
ZIPA.
CBE inatarajia kujenga majengo yake hapa Zanzibar tu taratibu za Uwekezaji kwa Chuo hicho utakapokamilika.Mkurugenzi ZIPA , Saleh Saad Mohamed (kulia), akizungumza na ujumbe kutoka Chuo cha Biashara CBE) kuhusu ujenzi wa hicho utakao fanyika maeneo huru ya Uwekezaji Fumba. Zanzibar.
No comments:
Post a Comment