Wizara ya Fedha imeibuka Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara
zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Aidha, Taasisi yake ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Ununuzi (PPRA) imeshika nafasi ya Kwanza kwa Upande wa Mamlaka za Udhibiti
nchini, huku Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA), ikishika nafasi ya Pili katika
kundi la Taasisi za Serikali.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya
Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, akiitazama Tuzo ya ushindi wa pili wa Jumla kwa
upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar
es Salaam yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja
vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya
Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba na Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Bi. Lilian Rugaitika, wakiwa wameshika Tuzo ya Mshindi
wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa
ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yalifanyika katika Viwanja
vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya
Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, baada ya Wizara ya Fedha
kuibuka na Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki
Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na
TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere,
Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Timu ya ushindi kutoka Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha, wakishangilia Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya
Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Chuo
cha Uhasibu Tanzania (IAA) baada ya Wizara ya Fedha kushinda Tuzo ya Mshindi wa
Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya
Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja
vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Kinondoni, wakishiriki kwa
furaha ushindi wa Wizara ya Fedha baada ya kuibuka Mshindi wa Pili wa Jumla kwa
upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar
es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.Picha ya Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara
zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya
TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa
Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024, ambapo Wizara ya Fedha imekabidhiwa
Tuzo hiyo baada kushinda nafasi ya Pili ya Banda Bora katika Maonesho hayo.
Picha ya Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara
zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya
TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa
Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024, ambapo Wizara ya Fedha imekabidhiwa
Tuzo hiyo baada kushinda nafasi ya Pili ya Banda Bora katika Maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment