Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefungua kongamano la uhifadhi wa mazingira ya bahari kwa visiwa vidogo vidogo vilivyowekezwa Zanzibar
………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefungua kongamano la uhifadhi wa mazingira
ya bahari kwa visiwa vidogo vidogo vilivyowekezwa Zanzibar lililofanyika Golden
Tulip Kiembesamaki Zanzibar, liloandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji
Zanzibar (ZIPA) na USAID kupitia mradi wake wa Heshim Bahari.
Rais Mwinyi amesema ni jambo la kupongezwa kwa
kufanyika kongamano hilo hapa Zanzibar na ukizingatia Zanzibar ni kisiwa
kilichopata umaarufu duniani kutokana na uwepo wa mazingira asili ya fukwe za
Bahari na kusema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa
kutokana na uchafuzi wa mazingira ya bahari jambo ambalo linaarhiri sekta ya
Utalii na ukuaji wa kiuchumi.
Amesema mpango mkuu wa Serikali kupitia Dira ya
taifa 2050 imeliangalia kwa kina suala la Uchumi wa Buluu kama eneo la
kipaumbele katika masuala mazima ya Kukuza Uchumi wa Nchi kwa matumizi ya
rasilimali za Bahari katika sekta ya Uwekezaji wa mafuta na gesi na Uwekezaji
katika Maeneo ya bahari.
Nae Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi Uchumi
na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff amesema kongamano hilo ni fursa ya kujifunza
kwa pamoja hatua gani za kuchukua katika kuyalinda mazingira ya bahari katika
suala zima la Kukuza Uchumi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kukuza
Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Nd. Saleh Saad Mohamed amesema kwa mara ya Kwanza
kongamano hilo limefanyika Zanzibar na mategemeo kutowa uelewa katika masuala
ya utunzaji wa mazingira ya bahari na hasa Wawekezaji katika visiwa ambao
wamekua kipaumbele kwa Uwekezaji wa utunzaji mazingira ya asili.
Kongamano hilo limewashirikisha watunga Sera za
nchi na Wawekezaji lengo ni kupata maoni ya pamoja juu ya hatua za kuchukua
katika uhifadhi mazingira na Uwekezaji nchini.
No comments:
Post a Comment