Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt. Festo Dugange. Akifungua Mkutano wa mwaka kwa maafisa lishe wa mikoa na halmashauri nchini Julai 16,2024 Jijini Dodoma
..................................
Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt.
Festo Dugange amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha
wanatoa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe kama
zilizopangwa katika bajeti.
Akifungua Mkutano wa mwaka kwa maafisa lishe wa mikoa na halmashauri nchini
leo Julai 16,2024 Jijini Dodoma Dkt. Dugange amewataka wakurugenzi hao
kuhakikisha fedha hizo zinatumika kutekeleza shughuli za lishe na kucha tabia
ya kuelekeza fedha hizo kufanya mirati mingine.
“Baadhi ya wakurugenzi wamekuwa na tabia ya kupeleka fedha za utekelezaji
wa afua za lishe kwenye matumizi mengine hivyo ni maelekezo ya Serikali
kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa
afua za lishe zinatumika katika afua hiyo na si vinginevyo” amesisitiza Dkt.
Dugange.
Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya tathmini katika Halmashauri zote
zilizotenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe, ikibaini fedha
hizo kutumika nje ya utekelezaji huo haitasita kuwachukulia hatua wakurugenzi
hao.
Vilevile, amewataka Maafisa lishe nchini kuhakikisha wanaimarisha elimu ya
lishe kwa jamii kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu lishe bora kulingana na
makundi ya vyakula hasa kwa mama wajawazito, watoto na vijana balee ili kujenga
utamaduni wa kutambua umuhimu wa vyakula hivyo.
Pia, Dkt Dugange amewataka maafisa hao kuhakikisha wanasimamia miradi ya
afua za lishe kupitia halmashauri zao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na
Serikali ya kupunguza changamoto ya lishe nchini.
Aidha, amewataka kuhakikisha takwimu zinazokusanywa kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya ngazi ya jamii ni sahihi na zenye ubora ili ziweze
kutumika kufanya maamuzi katika ngazi
No comments:
Post a Comment