Shree Krishna Vaibhavam II, Hadithi Isiyosimuliwa ya Bwana Krishna, hatimaye ipo tayari kwa tamasha la siku tatu kuanzia Julai 5 hadi 7 katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Tanzania. Uzalishaji na utengenaji wa hadithi hii ulianza kama ndoto miaka miwili iliyopita, baada ya tamasha la jukwaa lililofanya vizuri la Shree Krishna Vaibhavam I, lililofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 10 Julai 2022 katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kwa kipindi cha miezi 20 iliyopita, timu ya washiriki 150, ikiongozwa na Bi. Priti Punatar na Bi. Sonal Ganatra, wamefanya kazi kwa bidii ili kufanya tamasha hili la leo kutokea na kufanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaki, ukumbi ambao zinafanyika burudani zenye hadhi kubwa zaidi nchini Tanzania. Kama alivyosema Bw. Yogesh Manek, Mwenyekiti wa Shree Goverdhannathji Haveli, "tunajivunia kufanikisha tamasha linalosimulia hadithi takatifu kupitia aina za ngoma za kitamaduni kutoka India kwa hadhira ya Tanzania, kukuza uelewa wa kitamaduni na kuthamini umoja kati ya nchi hizi mbili."
Katika uhusiano kati ya Tanzania na India, tunamkaribisha Mgeni Rasmi Mheshimiwa Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti - Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutoa maoni yake juu ya tamasha hili. "Nina furaha kushuhudia tamasha hili kubwa la kitamaduni na onyesho la kipekee la urithi wa Jamii ya Kihindi inayoishi hapa nchini Tanzania. India na Tanzania daima zimekuwa na uelewano, ushirikiano wa pande mbili kati ya watu wetu na uhusiano wa karibu katika biashara na shughuli za kiuchumi pamoja na kubadilishana masuala mbalimbali ya kitamaduni, na tamasha hili ni mfano mzuri wa urafiki wetu."
Kama Shree Goverdhanathji Haveli, lengo letu katika kufanikisha tamasha hili ambalo linafanyika kwa mara ya pili. Malengo yetu ni Kwanza, kuhamasisha marafiki zetu, familia, na majirani kuzingatia mafundisho ya Krishna na kuelewa kanuni za ulimwengu na Kihindu. Pili, kuhamasisha vijana wetu kushiriki katika utamaduni wetu na kuwapa uelewa wa kina wa maadili na mafundisho ya Kihindu kupitia maisha ya Bwana Krishna duniani. Tatu, kushiriki hadithi nzuri na Watanzania, na marafiki wa Tanzania.
Na hadithi hii itapatikana duniani kote kupitia Kituo cha YouTube cha Shree Goverdhannathji Haveli mnamo Julai 7, 2024.
Kile kinachofanya tamasha hili kuwa maalum ni kwamba ni kazi ya upendo; ushirikiano wa vipaji vya kucheza ngoma na muundo wake wa utengenezaji kwa kushirikiana na timu za mbalimbali zilizofanikisha hadithi hii kutoka India – chini ya uongozi na msaada wa Shree Goverdhannathji Haveli na wadhamini, wafadhili ambao kiukweli bila uwepo wao uzalishaji huu usingewezekana. Tamasha hili linawaleta pamoja watu kutoka kila sehemu wenye maisha, umri, na jamii ya India, kwa upendo wetu wa pamoja kujifunza kuhusu maisha ya Kiimani ya Bwana Krishna.
Kuhusu Shree Goverdhannathji Haveli, Tanzania.
Ilijengwa mnamo mwaka 2017, Shree Goverdhannathji Haveli, Dar es Salaam, imekuwa kituo kikuu cha utamaduni na shughuli za kidini kwa wafuasi wa Pushtimarg kwa waumini wote wa Afrika Mashariki. Shrinathji ni umbo la Mungu wa Kihindu, Bwana Krishna aliyetokea kama mtoto wa miaka saba. Shrinathji ni mungu wa Dhehebu la Vaishnav linalojulikana kama Pushtimarg maana yake (Njia ya Neema) iliyoanzishwa na Shri Vallabhacharya Shri Mahaprabhuji mwaka 1492 BK.
No comments:
Post a Comment