Aidha TCB imetambua fursa inayoletwa na maadhimisho hayo na hivyo , benki
imeimarisha nafasi yake katika ushindani wa soko kwa kutangaza bidhaa zake mpya
za kidigitali ambazo zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya wateja yanayoendelea
kubadilika kila maisha ya watanzania ambazoi ni ADABIMA na KIKOBA.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais alisisitiza umuhimu wa Maonyesho ya
SABASABA katika kuleta maendeleo ya kiuchumi. Alisema, “Maonyesho ya SABASABA
ni kielelezo cha ustawi na maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Yanathibitisha
moyo wa ujasiriamali na ubunifu wa Watanzania Kwa kuzileta pamoja biashara
kutoka sekta mbalimbali, na kuwa maonyesho haya hayaoneshi tu uwezo wa kiuchumi
bali pia yanachochea ushirikiano wa pamoja unaowezesha ukuaji wa uchumi.
Maonyesho ya SABASABA yanaendelea kuwa kilele cha maendeleo ya kibiashara
nchini, yanatoa fursa kwa sekta mbalimbali kujumuika pamoja wakiwafikia wateja
na wadau mbalimbali ambapo Ushiriki wa TCB katika maonyesho haya unathibitisha
dhamira yake kushiriki katika ukuaji wa uchumi na ujumuishi wa kifedha.
ADABIMA ni mpango wa utoaji dhamana wa ada ambao TCB imeshirikiana na
kampuni ya Metro Life Assurance ili kuwapa wazazi na walezi utulivu wa kiakili
ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba watoto wanaweza kuendelea na elimu yao
hata pale wazazi au walezi wao wanapofariki au kupata ulemavu wa kudumu, na
hivyo kulinda malengo yao ya kitaaluma.
Akizungumza wakati wa maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki,
Francis Kaaya, amesema, “Tunatambua umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga
kesho bora ya jamii yetu na kwamba ADABIMA inawapa usalama wa kifedha lakini
pia inalea ndoto na matarajio ya wateja wake na kufafanua kuwa, “Bidhaa hii ni
uthibitisho tosha wa dhamira ya TCB Benki ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja
kadiri ya mahitaji yao na kuwahudumia Watanzania wote kwa ujumla.”
Kwa upande wake, Pray Henry Matiri, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa
Bidhaa za Kidigitali (Digital Product Operations Officer) ameeleza kuwa,
“Kikoba ni zaidi ya fursa ya kidigitali, kwani Kikoba inabeba dhana pana ya
uwazi, ujumuishi, na usalama katika uwekaji wa akiba na usimamizi bora wa
kifedha.
KIKOBA ni bidhaa mpya, rahisi na yenye ufanisi ya kuweka akiba mtandaoni
inayoboresha dhana ileile inayotumika katika vikundi vilivyozoeleka vya kuweka
akiba na kukopeshana ,Bidhaa hii ya kidigitali na ya kifedha, ikiwezeshwa na
ushirikiano wa kimkakati ambao TCB ilifanya na kampuni za simu nchini,
inawawezesha wateja kusimamia fedha zao kwa urahisi kutoka viganjani mwao
Maonesho hayo ya biashara ya 48 yameanza tarehe 28 na ufunguzi rasmi
ulifanyika rasmi Julai 3 na Rais wa
Jamhuri ya msumbiji Filipe Jacinto Nyusi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ambapo zaidi ya nchi 26
zinashiriki na watu zaidi ya 3,000 watashiriki na mwaka huu mamlaka ya maendeleo
ya biashara Tantred imesema washiriki wameongezeka zaidi ukilinganisha na mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment