.........................................
Na Mwandishi Wetu
MSAJILI wa Hazina, Nehemia Mchechu,ulai 15, 2024, ametangaza kuwa mashirika yote ya umma nchini yataanza kuchapisha wazi taarifa zao za kifedha ili kuhakikisha kunakuwa na uwazi na uwajibikaji kwenye mashirika hayo katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kufanya mageuzi kwenye mashirika hayo.
Mchechu ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, kwenye kikao kilichofanyika hapa jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa kwa sasa taasisi za kifedha na kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa pekee ndizo zinazotakiwa kuchapisha taarifa za kifedha.
Hivyo, kwa sasa agizo hilo jipya litakwenda kwenye mashirika yote ambayo yanaendeshwa na Serikali.
Mchechu akasisitiza kwamba umma lazima uarifiwe kuhusu utendaji wa kifedha wa taasisi zote za umma, ambapo uwazi huo utaweka wazi ni taasisi zipi zitalipa gawio kwa Serikali na zipi hazitafanya hivyo.
No comments:
Post a Comment