Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza na baadhi ya watumishi wanawake wa Wizara ya Fedha, Wamiliki wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, walezi na watoto wanaolelewa katika kituo hicho, kilichopo Chamwino Mkoani Dodoma baada ya kutembelea na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula, vinywaji, nguo, fedha taslim na mahitaji mengine.
.....................................
Josephine Majura na Asia Singano WF, Dodoma.
Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha, (Golden Women), wameshauriwa
kuendeleza utamaduni wa kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji
maalumu ili kuwasaidia kufikia malengo yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi Jenifa Christian Omolo, ametoa ushauri
huo alipotembelea Kituo cha Huduma cha
SAFAAD, kilichopo Kijiji cha Membe,
Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Aliongeza kuwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali ni jambo zuri
hivyo ni vema utaratibu huo ukaendelea ili kuhakikisha wanawafikia makundi
mbalimbali ya watu wenye uhitaji.
"Niwapongeze Uongozi wa Golden Women kwa umoja wenu wa kujitoa kwa
hali na mali na kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa”alisema Bi. Omolo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha Bi.
Consolatha Maimu, aliahidi kuendelea kuwahamasisha Wanakikundi hao kuwa na
utaratibu wa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Naye Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred,
aliwashukuru Wanawake wa Kikundi cha
Golden Women kwa kufika Kituoni hapo na kupeleka mahitaji .
Naye mmoja wa wanufaika wa mahitaji hayo Bi. Florentina Aloyce, aliuomba
uongozi wa Kikundi cha Golden Women, kuendelea kuwa mabalozi kwa vikundi
vingine ili viweze kufika kituoni hapo ili waweze kupata mahitaji kwa kuwa bado
wana mahitaji mengi.
Katika kuelekea maadhimisho ya sherehe ya Umoja wa Wanawake, Wizara ya
Fedha, imetembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD kwa ajili ya kupeleka mahitaji
ikiwemo mahitaji ya shule, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine mbalimbali.
No comments:
Post a Comment