Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea na kuongea na watumishi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja mpakani Julai 10, 2024. |
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuph Juma Mwenda
amekutana na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja katika Kituo cha
Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga kilichopo mkoani Arusha kwa lengo la
kusikiliza kero zao ili ziweze kutatuliwa na kuwezesha urahisi wa ufanyaji wa
biashara mpakani hapo na kuongeza mapato ya serikali.
Akiongea na watumishi wa taasisi mpakani hapo, Kamishna Mwenda amesema
kwamba, lengo la ziara yake mpakani hapo ni kuwatembelea na kusikiliza kero
zinazowakabili ili kuweza kuzitatua na kurahisisha biashara mpakani hapo.
“Nmekuja kuwasikiliza na kuona changamoto mlizonazo na tuone namna gani
tunaweza kufanya nini ili hii OSBP itumike kurahisisha shughuli za biashara kwa
sababu biashara zikiwepo ndizo zinaleta makusanyo ya kodi na kuweza kuleta
maendeleo ya nchi”, alisema Kamishna Mwenda.
Ameongeza kuwa, Serikali inazithamini taasisi zote zilizopo mipakani na TRA
pia itaendelea kuonesha ushirikiano kwa taasisi nyingine za Serikali ili suala
la utendaji kazi mpakani hapo linakua zuri katika kurahisisha biashara.
Aidha, amezishukuru taasisi zote za serikali zinazoonesha ushirikiano wa
pamoja katika kuhudumia wasafiri na wasafirishaji mpakani hapo na ameahidi
kuendelea kushirikiana na taasisi hizo na amesisitiza kuwa, taasisi hizo
hazinabudi kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
mpakani.
Kwa upande wao wawakilishi wa taasisi zilizohudhuria mkutano huo
zimempongeza Kamishna Mkuu wa TRA kwa kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao
na wameahidi kutoa ushirikiano ili biashara mpakani hapo iwe rahisi.Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda akizungumza na watumishi wa taasisi mbalimbali katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea na kuongea na watumishi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja mpakani hapo Julai, 10. 2024. |
No comments:
Post a Comment