Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa ufafanuzi kuhusu uanzishwaji wa matumizi ya Sarafu za Kidijitali, bungeni jijini Dodoma.
...........................
Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
SERIKALI kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa sasa inaendelea na
hatua ya utafiti wa uanzishwaji wa matumizi ya Sarafu za Kidijitali za Benki
Kuu (Central Bank Digital Currency) hapa nchini.
Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad
Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Mhe
Dkt.Faustine Engelbert Ndugulile, aliyeuliza Serikali ina mpango gani wa kuanza
kwa matumizi ya Sarafu za Kidijitali (Central Bank Digital Currency) hapa
nchini.
Mhe. Chande alisema kuwa Benki Kuu imebaini kwamba, kama ilivyo kwa mataifa
mengi, uanzishwaji wa Sarafu za Kidijitali za Benki Kuu (Central Bank Digital
Currency), unahitaji kuanzishwa kwa uangalifu na umakini bila kuleta athari
hasi katika mifumo ya malipo iliyopo nchini na pia kuweza kutatua tatizo halisi
la malipo ambapo kwa sasa bado mifumo iliyopo nchini inakidhi hali halisi ya
uwezeshaji mwananchi kutuma fedha na kufanya malipo.
‘‘Soko letu bado linahitaji kuendelea kuboreshwa katika kuimarisha mifumo iliyopo
kwa kutumia vyanzo vinavyopatikana kwa urahisi na wananchi wengi (simu za
kawaida) tofauti na matumizi ya Sarafu za Kidijitali zinazoitaji matumizi ya
simu janja (smartphones),’’ alisema Mhe. Chande.
Mhe. Chande alisema kuwa nchi nyingi ikiwa ni pamoja na majirani zetu na
ukanda wetu bado wapo katika hatua hizi za awali za utafiti na kuboresha mifumo
ya malipo iliyopo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Serikali inaendela na utafiti kuhusu matumizi ya fedha za kielektroniki
kuangalia namna nchi inaweza kunufaika endapo itahamia kwenye matumizi ya fedha
za mfumo huo wa kielektroniki.
‘‘Utafiti unaendelea na sasa wanaangalia uzoefu katika mataifa ambayo yameanza kutumia fedha za kidigitali ikiwemo Nigeria na nchi za Asia na baada ya kukamilika hatua zitafuata kwa utaratibu unaofaa,’’ alifafanua Dkt. Nchemba.Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali kuhusu uanzishwaji wa matumizi ya Sarafu za Kidijitali, bungeni jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment