TMA NA CRDB ZAWANOA MAAFISA UGANI MBEYA, NJOMBE, IRINGA NA SONGWE - UMOJA BANKING BLOG

Home Top Ad

MABENK

Post Top Ad

Friday, 30 May 2025

demo-image

TMA NA CRDB ZAWANOA MAAFISA UGANI MBEYA, NJOMBE, IRINGA NA SONGWE

Untitled-2

2u

 Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi (TMA) Bw. Elias Elipiki, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maafisa ugani yaliyotolewa na TMA kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kupitia mradi wa Tanzania Agriculture Climate Adaptation Technology Deployment Project (TACATDP).

.................................................

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kupitia mradi wa Tanzania Agriculture Climate Adaptation Technology Deployment Project (TACATDP) wamewajengea uwezo Maafisa Ugani wa namna bora ya kutafsiri na kutumia taarifa za hali ya hewa hususani katika shughuli za kilimo.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi (TMA) Bw. Elias Elipiki, alisema mafunzo hayo yanawalenga Maafisa Ugani kwani wao ni daraja kati ya TMA na wakulima, hivyo mafunzo haya yanalenga kutoa elimu  ya namna sahihi ya kutafsiri taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka na kuwawezesha wakulima kufanya mipango sahihi juu ya shughuli za kilimo kwa msimu husika.

Aidha, Meneja Uhusiano kutoka CRDB ambaye pia ni msimamizi wa utoaji wa mikopo inayozingatiwa uhifadhi wa mazingira katika mradi wa (TACATDP) Bw. Karim Kindole,  alisema CRDB na TMA wana ushirikiano katika kuwajengea uwezo Maafisa Ugani namna ya kudhibiti na kuwasaidia wakulima kupata taarifa sahihi za mabadiliko ya hali ya hewa.

Naye, Afisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Sostenesi Silayo, aliwashukuru TMA na CRDB kwa kuwapa nafasi Maafisa Ugani kupata elimu ambayo wataitumia katika kuwashauri wakulima kulima kilimo sahihi kutokana na hali ya hewa husika na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mengi.

1u

Mafunzo kwa vitendo yakiendelea kutolewa kwa maafisa ugani hao.

3u
Meneja Uhusiano kutoka CRDB ambaye pia ni msimamizi wa utoaji wa mikopo inayozingatiwa uhifadhi wa mazingira katika mradi wa (TACATDP) Bw. Karim Kindole, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
4u
Mafunzo kwa vitendo yakitolewa.
5u
Mafunzo yakiendelea.
6u
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wanaotekeleza mradi huo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *