NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI.42.4 KIGOMA,WADAU WAHIMIZWA KUUNGA MKONO SERIKALI - UMOJA BANKING BLOG

Home Top Ad

MABENK

Post Top Ad

Sunday, 4 May 2025

demo-image

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI.42.4 KIGOMA,WADAU WAHIMIZWA KUUNGA MKONO SERIKALI

Untitled-2

bangwe

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba  amepokea Vifaa vyenye thamani ya shilingi Mil.42.4 kwa ajili ya huduma za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha kwa Jamii.

Akipokea vifaa hivyo Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na miundombinu hiivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi. 

“Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwemo Afya na Elimu” amesema.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu meneja wa NMB kanda ya Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, Viti  vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia  ambavyo vyote vimetolewa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda hamsini (50) kwa Wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Hata hivyo, vifaa vya Afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha Afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *