Benki ya CRDB imetangazwa kuwa moja ya taasisi
zinazolipa kodi zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2023/2024 katika tuzo za
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinazotolewa usiku wa kuamkia leo katika
ukumbi wa The Super Dome Masaki ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alieambata na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick
Nshekanabo. Tuzo hii ni muendelezo wa kutambuliwa kwa benki ndani na nje ya
nchi ambapo kwa mwaka 2024, Benki ya CRDB imepata tuzo zaidi ya 50 katika
nyanja mbalimbali.
No comments:
Post a Comment