...............................................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENKI ya Taifa ya NBC
imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika
utendaji kazi wake ili kuhakikisha inakusanya Kodi kikamilifu kutoka kwao maana
wao ni miongoni mwa wadau wakubwa wanaoichangia TRA katika Kodi.
Akizungumza leo Tarehe 23.12.2024 baada ya
kupokea Salam za Shukrani kutoka kwa Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma
Mwenda zilizowasilishwa na Mkurugenzi wa Fedha wa TRA BI. Dina Edward Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Rayson Foya ameishukuru TRA kwa
kutambua mchango wao.
Foya amesema NBC itaendelea kutatua changamoto
za malipo kwa upande wao kwa kuboresha mifumo huku akibainusha kuwa wameshakuza
mifumo yao ya TEHAMA.
Kwa upande wa Benki ya HABIB mwakilishi wake Bw.
S. S. Hasan Rizvi ameishukuru TRA kwa kuisaidia benki yao kupitia mifumo GPG na
kuahidi kuendelea kushirikiana na TRA katika kukuza mapato ya serekali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha Bi. Dina
Edward akiwasilisha salamu hizo amesema Kamishna Mkuu anazishukuru Benki hizo
kwakua ni miongoni mwa benki za makusanyo ambazo zinazingatia matakwa ya
mkataba na TRA.
Amesema TRA kwakutambua mchango wa Benki hizo
Desemba ukiwa ni mwenzi wa shukurani wamekabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni
kutambua mchango wao ambao unapelekea huduma kwa wepesi.
No comments:
Post a Comment