BENKI YA CRDB YAZINDUA SAMIA INFRASTRUCTURE BOND - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 November 2024

BENKI YA CRDB YAZINDUA SAMIA INFRASTRUCTURE BOND

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango (katikati), Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi huo.

................................ 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 Benki ya CRDB imeweka historia kwa kufanya uzinduzi wa hatifungani ya miundombinu ya Samia Infrastructure Bond iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Katika uzinduzi hiyo yenye lengo la kukusanya Shilingi bilioni 150, Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali walihudhuria hafla hiyo wakiongozwa na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila. Benki yetu iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela.

Hatifungani hii ya kihistoria inalenga kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara za vijijini na mijini zilizopo chini ya wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA).

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweka ahadi ya kuwekeza kiasi cha Shilingi Milioni 200. 

Kwaupande wake Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango alitoa ahadi ya kuwekeza Shilingi Milioni 100 katika hatifungani hiyo. Jumla ya ahadi za takribani Shilingi bilioni 37 zilitolewa na taasisi, vikundi, na watu binafasi zilitolewa katika hafla hiyo.

Tunawakaribisha Watanzania wote taasisi, makampuni, wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa kawaida kuja kuwekeza katika hatifungani hii inayotoa faida nzuri ya asilimia 12 kwa mwaka kwa muda wa miaka mitano. Kiwango cha kuwekeza ni kuanzia Shilingi 500,000.

Unawekeza kuwekeza kidijitali kupitia SimBanking, au tembelea matawi yetu zaidi ya 260 kote nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango, akihutubia kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Hafla ya uzinduzi ikiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages